MKASA WENYE KUGUSA, JAMAA APATA SHIDA KUOA MWANAMKE KIPOFU
Mwanaume mmoja tajiri alikuwa anataka kuoa, lakini hakujua atamuoa nani maana kila msichana alikuwa akijisogeza sogeza kwake naye aliogopa kutokana na kizazi hiki kilicho jilaani chenyewe.
Basi akaamua kumuomba MUNGU ili aweze kumfungua macho ya rohoni aweze kumuona mwanamke sahihi wakumuoa.
Baada ya maombi yake ya wiki nzima siku ya jumapili akaenda Ibadani, akiwa hapo kanisani wakati wa maombi akamkumbusha MUNGU juu ya ombi lake. Ndipo MUNGU akamuonyesha msichana mmoja maskini na kipofu anaye sali naye humo kanisani.
Kisha MUNGU akasema: "Unatakiwa umuoe uyo msichana kipofu"
Jamaa akakataa nakuacha kuomba kabisa kwa muda uo, lack alipofika nyumbani jioni akapiga tena magoti nakuanza kumlilia MUNGU amuonyeshe mwanamke sahihi wakumuoa. Lakini hakujibiwa, akarudia kuomba Mara nyingi kila jioni. Ata ivyo kila baada ya maombi alionyeshwa msichana yule yule kipofu.!
MUNGU aliendelea kumuonyesha kuwa yule mwanamke kipofu ndio mkewe.
Basi kishingo upande huku akiamini uenda aliyempa majibu ni shetani, akaamua kukubali kumuoa uyo msichana kipofu.
Mipango ya ndoa ikafanyika na kila kitu kikawa sawa huku jamaa akiwa hana Amani kabisa.
Basi siku ya harusi wakiwa wamesimama mbele ya umati Mkubwa wa watu ndugu jamaa na marafiki.
Mchungaji akasema: "Tunaomba umfunue iyo shella ili umtazame kama ni yeye"
Macamera man, wapambe, na kila aina ya mbwembwe walijiandaa kuchukua picha ili waweke historia ya Kijana yule tajiri kuoa msichana kipofu na maskini.
ILE KUMFUNUA, MSICHANA YULE AKAINUA USO WAKE, DAAH! ALIKUWA KABADILIKA GHAFLA ALIKUWA ANANG'AA KAMA MWEZI KISHA AKAFUNGUA MACHO YAKE ANGAVU NA MAZURI. KISHA AKATABASAMU BAADA YAKUONA UMATI WA WATU WAKIWA NA ZAWADI ZA KILA AINA.
Jamaa hakuamini akapiga magoti nakuanza kumuomba MUNGU msamaha, kwa kumlaumu kwake baada yakumuonyesha uyo msichana.
NA KUANZIA SIKU IYO UYO MSICHANA HAKUWA KIPOFU TENA..!
UJUMBE:
Mungu anajua kwanini amekuchagulia icho kitu ulicho nacho, na anajua kwanini amekuweka katika hali au nafasi iyo uliyonayo sasa acha kulalamika.
MAOMBI YANGU KWAKO:
"Nakuombea kabla ya mwaka huu kuisha, Mungu akujibu maombi yako majibu ambayo yatawaacha adui zako vinywa wazi katika jina la Yesu kristo kwa imani wote tuseme Amen."
Kwa imani yako na dini yako, Koment neno AMEN, kisha share katika magroup yako ata kama ni magroup ya ngono wewe share tu maana kwa kufanya ivyo unavuna Baraka nakujiweka karibu na MUNGU zaidi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: