HIKI HAPA KISA CHA JOGOO ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSUMBUA MAJIRANI

Corinne Fesseau akiwa na jogoo wake

Jogoo huyu ambaye mmiliki wake alimpatia jina la Maurice, na akawa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri na kujikuta anafunguliwa mashtaka katika mahakama moja nchini Ufaransa.

Alilaumiwa kwa kusababisha kalele na familia moja katika kisiwa cha Oléron huko Ufaransa.

Mmiliki wake, Corinne Fesseau, alisema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya 'kuwikaa'.

Waliomshtaki Maurice na Maurice mwenyewe hawakufika mbele ya mahakama ya mji wa magharibi wa Rochefort siku ya kesi ilipoanza kusikilizwa.

Lakini jogoo huyo ambaye alijichukulia umaarufu kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili, alipata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama.

Walalamishi, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, walijenga nyumba yao mapumziko katika kijiji cha Saint-Pierre-d'Oléron karibu miaka 15 iliyopita, lakini baadae wakaigeuza kuwa nyumba ya kuishi walipostaafu.

Sababu moja iliyowafanya kuchagua sehemu hiyo ni utulivu wake lakini tatizo ni kuwa jogoo Maurice, alikuwa kero kwao kwani alikuwa akiwapigia kelele kila aalfajiri anapowika.

Wanasema tatizo hilo lilianza tangu mwaka 2017 jirani yao alipomnunua.

Walipowasilisha lalama zao kwa Bi Fesseau, ambaye aliishi Oléron kwa miaka 35, mabishano makali yalizuka mpaka mzozo kati yao ukagonga vichwa vya habari ulipofikishwa mahakamani.

Bi Fesseau, na majirani zake wengine, walisema hakuna mjadala kuhusu swala hilo - kwa sababu ufugaji wa kuku ni sehemu ya maisha ya vijijini na kwamba hawaelewi kwa nini walalamishi wanaomba jogoo huyo azuiliwe kuwika.

Chanzo - BBC

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.