HABARI MPYA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA KLABU YA YANGA, UONGOZI WATOA TAMKO KALI



UONGOZI wa klabu ya Yanga umetamba kuwa moto walioanza nao kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu hauzimiki, bali wataendelea kukusanya pointi tatu katika kila mchezo ulio mbele yao ili kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Yanga wameanza vizuri msimu huu ambapo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ndio vinara wa msimamo, wakiwa wamejikusanyia pointi 15 baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao mitano waliyocheza.

Mchezo ujao wa Yanga ni wa ugenini dhidi ya Namungo utakaopigwa Novemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Akizungumza hivi karibuni Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kwetu sisi nguvu kubwa tumewekeza katika timu yetu kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mchezo ulio mbele yetu ili kufanikisha dhumuni la kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

“Tunajua ligi ya msimu huu ni ngumu, lakini tunajivunia ubora wa kikosi tulichonacho ambao kwa kiasi kikubwa tuna uhakika kinaweza kutimiza malengo tuliyojiwekea.”

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.