ALIYEMTUNGUA DIARRA AFUNGUKA..ADAI IMEPUNGUZA MACHUNGU...

KIPA Diarra Djigui wa Yanga alikuwa hajatunguliwa tangu msimu uanze katika mechi za mashindano, lakini juzi alikumbana na kiboko yake, Shaaban Msala wa Ruvu Shooting aliyeweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kumtibulia kipa huyo kutoka Mali na kufunguka furaha aliyonayo kwa sasa.

Msala alisema licha ya chama lake kufungwa mabao 3-1, lakini kumtungua Diarra kumempungizia machungu.

Mfungaji huyo aliyekwamisha mpira dakika ya 9 ya mchzo alisema kabla ya kumtungua Diarra alisoma wasifu wake, ambao unamtambulisha namna alivyo hodari katika kuokoa michongo ya washambuliaji, hivyo kuzitikisa nyavu akiwa langoni kumempoza machungu.

“Ni kweli Diarra ni kipa mzuri, ila nimefurahi kuwa wa kwanza kumtungua ili apate changamoto ya namna soka la Tanzania lilivyo na ushindani wa hali ya juu,”alisema na aliongeza;

“Kwanza kufungwa kumetokana na mchezaji mwenzetu kulimwa kadi nyekundu, hivyo mfumo wa uchezaji wetu ule wa pasi nyingi, ukabadilika na Yanga wakatumia nafasi hiyo kutuadhibu,” alisema.

Alisema kumfunga Diarra wa kwanza akiwa kwenye timu bora nimeweka historia ambayo imeibua jina langu na nilichokifanya naamini kitafanya wadau wa soka wanifuatilie anahidi kuendelea kuwa imara zaidi ili kuwathibitishia kuwa sijabahatisha.

Msala aliongeza wamekutana na timu iliyo bora japo na wao walikuwa bora lakini kadi nyekundu iliwaondoa kwenye mipango ya kocha lakini wanatumia mapungufu waliyoyaonyesha dhidi ya Yanga ili kufanya vizuri mchezo ujao.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.