ALICHOKISEMA BERNARD MORRISON BAADA YA KUSHINDA KESI DHIDI YA YANGA
"Kuna mwanzo na mwisho wa kila kitu, hakuna kinachodumu milele, Tumekuwa tukisubiri hukumu (iwe nzuri au mbaya) mwisho umefika na kumaliza dukuduku.
Nataka kila mmoja ajue jinsi nawashukuru Yanga kwa kunipa nafasi na kuvaa jezi yao, hakuna mtu hapa Tanzania aliyenijua wala kujali kuhusu kipaji changu hadi kocha Luc Aymael aliponileta nicheze. Asante sana kocha kwa kuniamini na kunifanya mchezaji mkubwa. Kuna msemo Ghana unasema ' Dokta mbaya anayekupa huduma hadi dokta mzuri akafika anahitaji kupongezwa' hata kama alikuwa mbaya alikufanya uwe hai hadi yule mzuri alipofika. Kwahiyo rasmi niseme nawashukuru Yanga na yeyote aliyenifanya nitabasamu na kunipenda nikiwa Yanga, bila kusahau upendo wa mashabiki,"
Chanzo: Mwanaspoti
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: