ALIYEJIKATA UUME KWA WEMBE BAADA YA KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME AFARIKI DUNIA
Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amefariki dunia baada ya kuukata uume wake kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alipoteza nguvu za kiume.
Inaelezwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo wa kuukata uume wake baada ya kupata ajali na kuteguka kiuno na kusababisha asiwe rijali.
Akizungumzia juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Daudi Ally amesema leo Jumatatu Novemba 22, 2021 Juma amefariki baada ya kupungukiwa maji pamoja na damu.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: