BAADA YA KUICHARAZA NA KITU KIZITO AZAM FC...KMC KUIFUTA 'KIBABE' MBEYA CITY...
Kikosi cha Timu ya KMC FC kitaondoka jijini Dar es Salaam kesho kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa siku ya Jumamosi Novemba 27 katika uwanja wa Sokoine.
Msafara huo wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni utahusisha wachezaji 21, benchi la ufundi pamoja na viongozi ikiwa ni katika kuhakikisha timu inakwenda kupata matokeo mazuri katika mchezo huo licha ya kuwa KMC FC itakuwa ugenini.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia kitengo cha Habari imesema,
Hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri tangu kumalizika kwa mchezo wa mzunguko wa sita wa Ligi ya NBC dhidi ya Azam uliochezwa Novemba 21 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 Timu iliendelea na maandalizi jana jioni.
Licha ya kwamba mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa, lakini Benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Mkuu John Simkoko na wasaidizi wake Habibu Kondo pamoja na Hamadi Ally linaendelea kujiimarisha zaidi kuelekea katika mchezo huo na kwamba malengo na mikakati nikupambania Timu iweze kupata ushindi muhimu.
Lakini pia zaidi tunamshukuru Mungu kuwa katika mchezo uliopita hatukupata mchezaji mwenye majereha kwahiyo kikosi chote kipoimara na morali pia ipo juu, kikubwa mashabiki zetu waendelee kutusapoti kama ambavyo sikuzote wamekuwa wakifanya, tunahitaji kupambana zaidi ilikutoka kwenye nafasi ambazo tupo kwa hivi sasa.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: