WANAFUNZI 393 WAFUTIWA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2021..TAZAMA MATOKEO HAPA


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde
**

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 393 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2021.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 30, 2021, na Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dkt. Charles Msonde, na kusema kwamba NECTA imezishauri mamlaka zinazohusika, kuwachukulia hatua kwa mujibu wa kanuni za utumishi na sheria za nchi wale wote waliohusika ama kusababisha kutokea kwa udanganyifu huo.

Aidha Dkt. Msonde akizungumzia ufaulu amesema kwamba, idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa mwaka 2021 imeongezeka kwa watahiniwa 74, 130 sawa na asilimia 8.89 ikilinganishwa na mwaka 2020, ambapo somo la Kiswahili limeongoza kwa wanafunzi kufaulu huku ufaulu katika somo la English ukishuka na kuwa na asilimia 48.02.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.