HIKI NDIO ALICHOKISEMA MWIJAKU KUHUSU KUTEMBEA UCHI BAADA YA SIMBA KUFUNGWA JUZI...


MHAMASISHAJI wa Klabu ya Simba, Mwijaku amegoma kufanya kile alichoahidi hivi karibuni kwa mashabi wa Simba mbele ya waandishi wa habari, baada ya kutoa kauli yake ya kwamba angetembea utupu bila nguo, endapo Simba ingepoteza katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Mwijaku amedai kwamba alikua tayari kutekeleleza ahadi yake lakini amejua kwamba sheria ya nchi haimruhusu kufanya hivyo.

Ikumbukwe klabu ya Simba imeondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu na Jwaneng Galaxy ya Botswana baada ya kuruhusu kufungwa bao 3-1 nyumbani kwenye mchezo wa juzi jumapili katika dimba la Benjamin Mkapa.

Hayo yanajiri baada ya Simba kuruhusu kufungwa mabao matatu nyumbani na kufanya uwiano wa mabao kuwa 3-3 baada ya kushinda 2-0 ugenini hivyo wameondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.