BI HARUSI BILIONEA AFARIKI AKIWA HONEYMOON, SIKU YA TATU BAADA YA NDOA
Bi Julia Donson Wachira (73), mke wa kijana mkenya ameripotiwa kupoteza maisha akiwa honey moon ikiwa ni siku tatu mara baada ya kufunga ndoa na kijana huyo wa miaka 34.
Mama huyo anayedaiwa kuwa tajiri wa kutupa akiacha mabilioni ya fedha katika akaunti zake anadaiwa kufunga ndoa na kijana John Wachira ambao walikuwa wakiishi huko Florida nchini Marekani.
Katika kile kinachoonekana kuumizwa na msiba huo mume wa mama huyo Bw. John Wachira ameandika kuelezea majonzi yake kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Face book. ”Kipenzi cha maisha yangu hayupo tena, amefariki jioni hii, ningetoa kila kitu kumrudisha” ameandika.
Ndoa yao ilikuwa na tofauti kubwa ya kiumri ambapo mama huyo alikuwa akimzidi kijana huyo miaka thelathini na tisa. Licha ya kuacha kiasi kikubwa cha fedha pia mama huyo anadaiwa kuacha majumba ya kifahari na makampuni.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: