HUU HAPA MCHONGO MPYA WA KLABU YA SIMBA, ATCL WAWAPA DILI
UONGOZI wa Klabu ya Simba SC na Shirika la Ndege nchini Tanzania (ATCL) wameingia mkataba wa ushirikiano wa kibiashara ambao utakuwa na manufaa kwa pande zote.
Mkataba huo utaiwezesha Simba kuweza kusafiri ndani ya Tanzania kwa ndege za shirika hilo pekee ikiwa katika safari zake.
Inatajwa kuwa mkataba huo uana thamani ya shilingi milioni 400.Mkataba huo umesainiwa leo Septemba 17 mbele ya Waandishi wa Habari.
Mkataba ambao wamesaini leo ni wa muda wa miaka miwili kwa ajili ya ushirikiano.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: