YANGA YAKIRI KUWA MCHEZO WA RIVERS UNITED HAUTAKUWA MWEPESI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba mchezo wao wa marudio dhidi ya Rivers United hautakuwa mwepesi ila wamejipanga kuweza kufanya vizuri.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Rivers United kwenye mchezo wa marudio.

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa nchini Nigeria Septemba 19.

Katika ule mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-1 Yanga hivyo kazi kubwa ipo kwenye kupindua matokeo ugenini.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema:"Tunajua mechi za ugenini zina visa na mikasa mingi, tumejipanga na tumejiandaa na hilo na ndiyo maana tulituma watu imara wakufanya maandalizi yote kabla ya timu kufika.

"Tunaenda kucheza mechi ambayo kwa vyovyote vile itakuwa ngumu, mechi za ugenini kwenye ligi ya mabingwa siku zote huwa ni ngumu na hilo jambo tunalitarajia," .

Ni Senzo Mbatha ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Yanga kwa muda aliweza kutangulia nchini Nigeria na kwa sasa yupo huko akisubiri kuwapokea Yanga.

Mbatha ameweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa licha ya changamoto za soka la Afrika ambazo huwa hazikosekani.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.