JINSI DIWANI WA CHADEMA ALIVYOFUKUZWA KWENYE KIKAO AKIWATUHUMU MADIWANI WA CCM KUHONGWA SHINYANGA
Kushoto ni diwani wa Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi (CHADEMA),Kulia ni diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila (CCM)- Picha na Maktaba ya Malunde1 blog)
Hali ya taharuki imezuka katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga baada ya naibu mstahiki meya wa manispaa hiyo Agnes Machiya kutoa agizo kwa kamati ya ulinzi na usalama kumtoa nje na kutomruhusu kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila posho diwani wa kata ya Ngokolo Emanuel Ntobi (CHADEMA) akituhumiwa kusambaza taarifa ya uongo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akiwakashfu madiwani wa CCM.
Ntobi anadaiwa kuwakashfu madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wamehongwa vitenge ili wapitishe kuipitisha bajeti iliyokuwa imeletwa kwenye kikao cha kwanza baada ya kuonekana ina mapungufu.
Machiya ametoa agizo la Ntobi kutolewa kwenye kikao leo Januari 16,2018 kwenye kikao cha pili cha mapendekezo ya kupitisha bajeti 2018/2019 kufuatia madiwani jana kuunga mkono hoja ya kuikataa bajeti ya 2018/19 iliyopelekwa na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga.
Wakati kikao cha leo kikiendelea baadhi ya madiwani wa wa CCM akiwemo diwani wa viti maalum Zuhura Waziri na Hassan Mwendapole walieleza kufedheheshwa na kudhalilishwa na taarifa ya Ntobi kuwa madiwani wa CCM wamehongwa vitenge.
Kufuatia malalamiko ya madiwani hao ndipo Naibu Meya Machiya akalazimika kumtoa nje diwani Ntobi na kutoruhusiwa kuhudhulia vikao vitatu mfululizo kutokana na kusambaza ujumbe wa uongo mtandaoni akimtaka aende sehemu yoyote akashtaki.
Baadhi ya maneno yaliyosomeka katika taarifa ya Ntobi mtandaoni aliyoipost jana usiku ni “Nazo taarifa Madiwani wa CCM usiku huu wamekwisha kuhongwa "Vitenge" ili kesho mambo yawe sawa tafadhalini KATAENI.Heko Madiwani CHADEMA”.
Akiongea kwa hasira huku akipiga meza kwa nguvu baada ya kugoma kutoka kwenye kikao na kuomba apewe nafasi ya kuongea siyo kumhukumu bila utaratibu Ntobi,alidai anaoushahidi wa kutosha wa sauti na picha ukionesha madiwani wa CCM wakipokea rushwa ya vitenge ili bajeti ipitishwe na hata wakimpeleka sehemu yoyote atautoa.
Baada ya Ntobi kugoma kutoka katika kikao hicho,Naibu Meya alimwamurisha askari aliyekuwa katika kikao kumtoa diwani huyo,hali iliyomlazimu Ntobi atii amri na kuvua joho kisha kutoka nje ya ukumbi huku akisindikizwa na askari huyo.
Katika hali iliyoonesha kuwepo kwa sintofahamu katika baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga,mbali na Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi(Chadema) kupost taarifa mtandaoni,jana Diwani wa Kata ya Ndembezi David Nkulila (CCM) naye alipost ujumbe wenye utata katika ukurasa wake wa Facebook huku akipost picha akiwa na Ntobi.
Sehemu ya ujumbe huo wa Nkulila inasomeka “TAARIFA ZA UONGO,,,,,,,, zina sifa ya ya Big G, a.ka JOJO, wa kale waliita BAZOKA, utafurahia utamu unapoanza kutafuna tu,,,, mwisho utaitema……..SIPENDI KUDANGANYWA,,,!!! Kwanini nami niseme uongo kwa watu.!!?? Tena wanao Kuheshimu!! DHAMBI MBAYA. * KITAELEWEKA. *yes----nkulila na rafiki yangu ntoby.Good neighbor.(Ujirani mwema)Kata ya Ndembezi na Ngokolo.Together we can.Kesho BARAZA la Bajeti Linaendelea,,,,!”.
HUU NDIYO UJUMBE WA DIWANI WA KATA YA NGOKOLO, Emmanuel Ntobi ALIOUPOST FACEBOOK JANA JANUARI 15,2018
Wananzengo,
Napenda kuwashkru sana Waheshimiwa Madiwani wote, Waliounga mkono HOJA ya kuikataa Bajeti ya 2018/19, iliyoletwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Shinyanga.
Napenda kuwashkru sana Waheshimiwa Madiwani wote, Waliounga mkono HOJA ya kuikataa Bajeti ya 2018/19, iliyoletwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Shinyanga.
Kwa leo, ningeshanga sana Waheshimwa Madiwani kama mmeugana na Mkrugenzi ambaye ameleta "figure" tofauti za Mpango wa Bajeti wa Halmashauri yetu.
Kwamba, Mkurugezi kaleta Mapango wa Bajeti 2018/19 Mapato wa Ndani (own source) kuwa tofautia.
Kwamba tutakusanya,
(1) Tsh 2.4 Bilioni,
(2) Tshs 2.8 Bilioni na
(3) Tshs 3.0 Bilioni.
(1) Tsh 2.4 Bilioni,
(2) Tshs 2.8 Bilioni na
(3) Tshs 3.0 Bilioni.
Hongereni kuwatendea HAKI wanaShy.
Nawaomba Kesho tuendelee kuwa na msimamo wa kupinga, wafanyabiashara wenye vibanda Ngokolo Mitumbani na kwingine kupandishiwa kodi kutoka Tsht 10, 000/= kwenda Tshs 50,000/=
Tupinge kwa Nguvu zote, ushuru wa meza sokoni (WauzaMchicha), kutoka Tshs 200/= na kuwa Tshs 500/=
Nazo taarifa Madiwani wa CCM usiku huu wamekwisha kuhongwa "Vitenge" ili kesho mambo yawe sawa tafadhalini KATAENI.
Heko Madiwani CHADEMA.
Wasalaaam,
E.Ntobi
Diwani Ngokolo.
E.Ntobi
Diwani Ngokolo.
UJUMBE WA David Nkulila KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK
TAARIFA ZA UONGO,,,,,,,, zina sifa ya ya Big G, a.ka JOJO, wa kale waliita BAZOKA, utafurahia utamu unapoanza kutafuna tu,,,, mwisho utaitema.
Ahaaa,,,,, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, watu wanapenda kuambiwa ukweli, na Kuwaambia watu ukweli, hata kama ukweli huo unauma kiasi gani!! Ni ishara ya kuwaheshimu. Kuwaambia watu wazima uongo, huku ukijua unawadanganya!! Ni kuwadharau na kuwafanya kama watoto wadogo, tena wajinga na wapumbavu!!! Alimaliza Mwl Nyerere. Nakubaliana naye saana.
SIPENDI KUDANGANYWA,,,!!! Kwanini nami niseme uongo kwa watu.!!?? Tena wanao Kuheshimu!! DHAMBI MBAYA.
* KITAELEWEKA.
*yes----nkulila na rafiki yangu ntoby.
Good neighbor.
(Ujirani mwema)
Kata ya Ndembezi na Ngokolo.
Together we can.
Kesho BARAZA la Bajeti Linaendelea,,,,!
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: