HARMORAPA AFUNGUKA TENA MENGINE KUHUSU WEMA SEPETU
Msanii wa muziki Harmorapa amefunguka kuhusu post aliyoweka katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuhusiana na Dk.Shika na mrembo Wema Sepetu.
Akipiga stori na Bongo5, hivi karibuni msanii huyo ameeleza kuwa wakati tukio la Dk.Shika linataokea yeye hakuwepo nchini.
“Kipindi kile wakati inatoke sikuwepo hapa nchini nilikuwa china kwa ajili ya biashara yangu, nikawa nasikia nikawa naona kinachoendelea hapa Tanzania home hapa nyumbani. Lakini kuhusu mimi kuwa baba yangu na kumpost watu wengi wanacheza na akaunti yangu wali hack one time harafu waka-post wakaandika kama walivyo andika lakini mimi sina uhusiano nao harafu sielewe kinachoendela, ukiniuliza leo hivi nashindwa hata kuelewa ,” amesema msanii huyo baada ya post yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram kudai kuwa ana mahusiano na tajiri mtata Dk.Shika.
Akaongeza” Watu wana hack tu sometimes kuniharibia yani na wanatumia vibaya mimi mwenyewe naumia na kujiuliza sasa kwa nini nikae kwenye mitandao na kumtukana mtu na ukimtukana mitandao ni vyombo vya habari kila mmoja ataisikia hivi ni kuharibiana inakuwa sio ishu sio poa kiukweli.”
Vile vile msanii huyo akasisitiza kuwa alimtaja Wema Sepetu katika post hiyo kwa sababu ni mrembo, akaongeza “ Anamtaja mrembo huyo kwa sababu anampenda .”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: