BOSI WA ZAMANI WA TSHISHIMBI AUAWA KWA RISASI
YANGA itacheza na Mwadui FC leo Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, lakini habari si njema kwa kiungo wake tegemeo, Papy Kabamba Tshishimbi, baada ya kupata pigo la kufiwa na bosi wake wa zamani, Victor Gamedze.
Gamedze, aliyekuwa mmiliki na Mwenyekiti wa klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland ambayo kiungo huyo alichezea kabla ya kujiunga Yanga, ameuawa kwa kupigwa risasi nchini humo.
Bilionea huyo, ambaye alikuwa mfanyabiashara na mdau mkubwa wa soka la Swaziland, alipigwa risasi juzi Jumapili saa moja usiku kwenye kituo cha kujazia mafuta cha Ezulwini Galp kilichopo jijini Mbabane muda mfupi baada ya kutazama mechi ya watani wa jadi nchini humo baina ya timu yake na Manzini Wonderers.
Ni kweli Mwenyekiti wetu ameuawa kwa kupigwa risasi. Wote tumeshtushwa na tukio hilo na kwa sasa tupo bize kuweka mambo sawa pamoja na familia. Tutatoa taarifa rasmi,” alisema Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Sandile Zwane, alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Independent
Mwanaspoti
Mwanaspoti
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: