MTANZANIA AFARIKI AKISAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga amethibitisha kupokea taarifa ya Mtanzania kufariki dunia akisafirisha dawa za kulevya.
Amesema alikuwa akisafiri kuelekea nchini China kwa ndege ya Shirika la Ethiopia na alizidiwa kutokana na dawa alizokuwa amemeza.
“Ni kweli kuna Mtanzania amekutwa amekufa kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia akiwa amemeza dawa za kulevya. Tunaendelea kufuatilia kujua jina lake na amezitoa wapi hizo dawa,” amesema.
Sianga akizungumza na MCL Digital leo Desemba 5,2017 amesema taarifa hizo walizipata jana na kwamba wanaendelea kufuatilia.
Amesema hivi sasa Watanzania wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya wengi wanatumika kupokea mizigo na kuisafirisha kunakohitajika.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: