MKURUGENZI WA WILAYA YA NKASI ATUMBULIWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi, Julius Kawondo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni

Jafo amewaambia waandishi wa habari jana Ijumaa kuwa Kawondo ameshindwa kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.

"Natumia Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na Sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo," alisema Jafo.

Alisema fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa Kijiji cha Kamwanda ambako mkurugenzi alishirikiana na mmoja wa maofisa kutoka wizara ya maji.

Jafo alimuomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi huyo kuhujumu mradi wa maji katika Kijiji cha Kamwanda wilayani humo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.