CUF YA MAALIM SEIF YAFURAHISHWA NA KITENDO CHA MBUNGE WA KINONDONI MAULID MTULIA KUJIUZULU UBUNGE
Chama cha wananchi CUF upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu Maalim seif sharif Hamad, kimesema Kimefurahishwasana na uamuzi wa aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, jijini Dar es Salam, Maulid Mtulia kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa Chama cha Wananchi CUF na kuhamia CCM.
Akizungumza na Masengwa Blog kwa njia ya simu Mkurugenzi Wa Uchumi Na Fedha Wa CUF ambaye ni Kaimu NAIBU MKUU Wa CUF Bara Mhe. Joran Bashange amesema;
''Hali halisi ni kweli kwamba Maulid Mtulia amejiuzulu kwa sababu ametoa statement kwenye vyombo vya habari, taarifa kwa umma na akaenda live na sasa habari zake zipo kwenye mitandao ya kijamii ambayo inathibitisha kuwa amejiuzulu karuka kaenda CCM''
Mh. Joran Bashange amesema kuwa CUF ya Maalim Seif kwa upande wao wamefurahishwa na kitendo hicho cha kujiuzulu na nafasi zote alizokuwa nazo ndani ya Chama hicho na kuhamia CCM
''Sisi kwetu habari hii tumeipokea furaha kubwa sana kujiuzulu kwake kwa sababu huyu mtu alikuwa kambi ya Lipumba waliokuwa wakitumika na CCM kutuvuruga kwa hiyo kama wameamua kujisalimisha kwenda, basi watuachie chama chetu salama na sisi tunamshukuru Mungu wetu sana na tunawashauri na wale wengine waondoke mapema sana ili watuachie chama chetu''
Mtulia alijiuzulu nafasi yake ya ubunge na kuhamia CCM hapo jana akidai kuwa kutokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya ubunge, na kusema “nimebaini kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza” alisema.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: