Video: SHUHUDIA MWANAMKE ALIYEFUFUKA MIEZI 6 BAADA YA KUZIKWA

Mwanamke, Chausiku Ndereme, aliyekufa miezi 6 iliyopita ameonekana tena akiwa hai huku akiwa amepigwa na bumbuazi kiasi cha kushindwa kuongea vizuri, ambapo mume wake January Kapera, amesema mara baad ya mke wake kufariki taratibu za mazishi zilienda vizuri. 

Pia amesimulia mazingira ya kifo cha mke wake huyo, siku hiyo baada ya kupata chakula cha usiku, aliingia chumbani na kumkuta yeye, ambapo baada ya muda alianza kupata maumivu ya kichwa, yalipozidi walimkimbiza hospitali na mara baada ya kufika akawa tayari ameshafariki, ndipo walipobeba maiti na kurudi nyumbani ambapo mchango ulipitishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki na akasafirishwa mpaka mkoani Shinyanga, ambapo ndipo alipozikiwa. 

Aidha Agness Leonard, ambaye amepanga nyumba moja na marehemu huyo, alisema kuwa siku ya tukio marehemu alipika vizuri ioni na akaingia ndani kwake kulala, mudaa mfupi baada ya kuingia ndani alisikia sauti ya mume wa marehemu akipiga kelele za kuomba msaada, haraka wakainuka na kukimbilia, walipofika wakamkuta mama huyo katoa ulimi na mapovu yanamtoka.
BOFYA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO YAKE

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.