SOFIA SIMBA ARUDISHWA CCM
Mkutano wa halmashauri kuu ya CCM Taifa umeridhia kumpokea Kada wa Chama hicho Sofia Simba ambaye alifukuzwa na chama hicho baada ya kubainika kukisaliti chama hicho kwa kumuunga mkono Edward Lowassa ambaye sasa ni kada wa CHADEMA. Mwenyekiti wa CCM taifa John Pombe Magufuli amesoma barua ya Sofia Simba kuomba radhi ambapo amesema aliandika barua nyingi za kuomba kusamehewa baada ya kukiri makosa yake na kwamba yeye amekulia ndani ya CCM hivyo hajisikii kuishi nje ya chama hicho. |
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: