MBWA ASIMAMISHA MECHI BOLIVIA...AKIMBIA NA MPIRA UWANJANI KATIKATI YA MECHI

Mbwa wa polisi amezua taharuki wakati alipoingia uwanjani na kukimbia na mpira wa mchezo wa kati ya Blooming dhidi ya Nacional de Potosi waLigi Kuu Bolivia.

Mbwa huyo wa polisi alifanikiwa kutoka mikononi mwa askari aliyekuwa amemshika na kuingia uwanjani wakati mechi ikiendelea kabla ya kuung’ata mpira na kukimbia.

Kitendo hicho cha mbwa kukimbia na mpira ukiwa mdomoni mwake kilisababisha mechi kusimama kwa sekunde 40.

Askali walianza kumkimbiza mbwa huyo uwanjani jambo lililofanya mashabiki wa watazamaji kupata burudani ya aina yake.

Mwisho mchezaji Alejandro Quintana anayechezea Blooming alifanikiwa kumkata mbwa huyo na mechi kuendelea.

Mwisho wa mechi hiyo Blooming ilifanikiwa kushinda kwa mabao 4-2, lakini mbwa huyo wa polisi ndiye aliyeshika vichwa vya habari.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.