KOCHA WA SIMBA AJPANGA KUVUNJA REKODI YA YANGA
Timu ya Simba haijawahi kushinda mechi mbili mfululizo kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, lakini safari hii kocha Joseph Omog ametamba kuvunja rekodi hiyo .
Kocha Omog ameandaa mpango mkakati maalumu ambao utakiwezesha kikosi chake kuibuka na pointi sita kwenye mechi mbili wanazokwenda kucheza Nyanda za Juu Kusini.
Akifafanua zaidi Omog amesema kuwa amepania kuhakikisha timu yake inavunja rekodi ya Yanga kwa kushinda mechi hizo mbili ingawa amekiri kuwa siyo jambo dogo.
“Msimu uliopita tulijitahidi kufanya hivyo lakini ilishindikana msimu huu tunaanza tena kucheza ugenini mechi zote mbili kwa ubora wa kikosi tulichokuwa nacho naamini tunaweza kuvunja rekodi ya Yanga”.
Omog amesema anaziheshimu timu za Mbeya City na Tanzania Prisons, lakini msimu huu ataomba wawasamehe kwani wamejipanga kuhakikisha wanarudisha heshima na hadhi ya Simba.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi