Duh!! ZANZIBAR HEROES WAENDA KENYA KWA BASI NA BOTI
KIKOSI cha Zanzibar Heroes, kimeondoka Unguja leo kwenda Kenya kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yanayotarajia kuanza Desemba 3, wakitumia usafiri wa basi na boti.
Msafara huo wa watu 34, wachezaji 24 na viongozi 10, wamendoka majira ya saa 3:00 asubuhi na boti ya Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam.
Wakifika Dar es Salaam, watapanda basi kwenda Kenya, wakipita njia ya Tanga.
Mkuu wa msafara, Khamis Haji: “
Matarajio ya safari yetu, itakuwa yenye matumaini kwani kila mmoja amejiandaa vema kwa ajili ya kuhimili mawimbi ya bahari pamoja na upepo wa njiani tutakapokuwa ndani ya mabasi.”
“Tumaini la safari yetu hii itakuwa yenye mafanikio makubwa kwa Zanzibar nzima, kikubwa tunaomba dua zenu tusafiri salama kwenda na kurudi,” alisema Kocha wa timu hiyo Hemed Suleiman ‘Morocco’.
Miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Ahmed Ali ‘Salula’, Nassor Mrisho, Mohammed Abdulrahman ‘Wawesha’, Abdallah Haji ‘Ninja’, Mohd Othman Mmanga, Ibrahimm Mohammed ‘Sangula’ , Adeyum Saleh ‘Machupa’, Haji Mwinyi Ngwali, Issa Haidar ‘Mwalala’, Abdulla Kheir ‘Sebo’, pamoja na Ibrahim Abdallah .
wengine ni Abdul-swamad Kassim, Abdul Aziz Makame, Mudathir Yahya, Mohammed Issa ‘Banka’, Amour Suleiman ‘Pwina’, Hamad Mshamata,
Suleiman Kassim ‘Seleembe’, Kassim Suleiman , Feisal Salum , Khamis Mussa ‘Rais’, Mwalimu Mohd, Seif Abdallah ‘Karihe’ na Ibrahim Hamad Hilika.
Awali wachezaji hao walikuwa 30 na kulazimika kuachwa 6 ambao wengine waliachwa kwasababu ya majeruhi akiwemo Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ) na Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege) huku wengine walioachwa ni Mbarouk Marshed (Super Falcon) na Omar Juma ‘Zimbwe’ (Chipukizi).
Hata hivyo kwa upande wa viongozi ambao wanaungana na wachezaji hao katika msafara wa kuelekea nchini Kenya kwa ajili ya mashindani ya Chaleng na Hemed Sulaman Morocco Kocha Mkuu, Ali Sulaiman Kocha Msaidizi, Khamis Haji Mkuu wa msafara, Abdul Wahab Dau Meneja wa timu, Mohamed Yussuf Daktar wa timu, Hafidh Muhidini Msaidizi wa shughuli za timu pamoja na Abubakar Khatib Mwandishi wa Habari.

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: