CHIRWA WA YANGA AMCHANGANYA JUUKO WA SIMBA...KISA HIKI HAPA





JUMAMOSI iliyopita Simba na Yanga zilikutana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1. Simba wakipata bao kupitia Shiza Kichuya wakati lile ya Yanga likifungwa Obrey Chirwa. 

Hata hivyo, baada ya mechi hiyo beki wa Simba raia wa Uganda, Juuko Murshid alijikuta katika wakati mgumu kutoka kwa baadhi ya viongozi na mashabiki wa timu hiyo wakimtuhumu kucheza chini ya kiwango na kushindwa kumzuia Chirwa kuifungia Yanga bao hilo lililokuwa la kusawazisha.

Kutokana na hali hiyo, hivi sasa Juuko anadaiwa kutumia muda mwingi akiangalia video ya bao hilo la Chirwa ili kujiridhisha kama kweli alifanya uzembe katika kumzuia Chirwa asifunge bao hilo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa, tangu siku hiyo Juuko amekuwa hana amani kama zamani kwani bado akili yake imetawaliwa na tuhuma hizo alizopewa baada ya mechi hizo za kushindwa kumzuia Chirwa.

“Mchezo wa soka ni mchezo wa makosa, Wanasimba wanapaswa kuelewa hivyo na siyo kuanza kuwatuhumu tu wachezaji, kwani hivi sasa Juuko hayupo sawa kabisa kama zamani kabla ya mechi ya Yanga. 

“Kwa sasa anatumia muda mwingi kuangalia video ya bao la Chirwa ili aweze kujiridhisha kama kweli uzembe ulikuwa wake.
“Kilichosababisha afanye hivyo ni kutokana na tuhuma ambazo amekuwa akitupiwa na baadhi ya viongozi pamoja na mashabiki wa timu hiyo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipotafutwa Juuko kuhusu suala hilo, hakuwa tayari kusema chochote lakini kocha wake mkuu, Joseph Omog alisema: “Hivi sasa yupo vizuri ila mwanzoni hakuwa sawa.”

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.