Breaking News : MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA CHADEMA TAIFA PATROBAS KATAMBI AHAMIA CCM



Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema (BAVICHA),Patrobas Katambi amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Katambi ametangaza kujiondoa Chadema leo Jumanne Novemba 21,2017 katika mkutano wa halmashauri kuu ya CCM unaoendeshwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.

Katambi alikuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akikabiliana na Stephen Masele (CCM) ambaye aliibuka mshindi huku Katambi akidai kuibiwa kura katika uchaguzi huo.

Mbali na Katambi makada wengine wa CHADEMA wameamua kurudi CCM.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.