BARUA YA SPIKA WA BUNGE KUHUSU LILILOKUWA JIMBO LA NYALANDU
Barua ya Spika wa Bunge kuhusu lililokuwa Jimbo la Nyalandu
MPEKUZI / 44 minutes ago
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo Novemba 3, 2017 amemuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) kumtaarifu kuwa jimbo la Singida Kaskazini lipo wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Taarifa ya Bunge iliyotolewa leo inasema kuwa jimbo hilo lipo wazi kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfuta Uanachama Lazaro Nyalandu toka Oktoba 30, 2017 siku ambayo Mbunge huyo alitangaza mwenyewe kupitia vyombo vya habari kujivua nafasi zake ndani ya chama hicho na kusema kuwa ameandika barua kwa Spika kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia CCM.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: