HIKI HAPA ALICHOKIONGEA AJIBU KWA WANASIMBA
Ibrahim Ajibu akifanya yake (Mwenye mpira).
MSHAMBULIAJI tegemeo hivi sasa wa Yanga, Ibrahim Ajibu amewaondoa hofu mashabiki kwa kutamka: “Waacheni watani wetu Simba wachonge na mwisho wa mechi watakaa kimya.” Kauli hiyo, ameitoa akiwa ametoka kufunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Stand United iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika ushindi wa mabao 4-0 huku mengine yakifungwa na Obrey Chirwa na Pius Buswita.

Nyota huyo alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika, akichota kitita cha shilingi milioni 50 na gari aina ya Toyota Brevis.
Akizungumza nasi, Ajibu aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo akidai wana kikosi imara kitakachopata matokeo mazuri ya ushindi kwenye mechi hiyo itakayochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ajibu alisema katika mechi hiyo atahakikisha anatengeneza au anafunga bao katika mechi hiyo ili iwe shukrani kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kumpokea vizuri tangu atue Jangwani.
“Mechi hii dhidi ya Simba ni muhimu kwetu kupata pointi tatu ili tukae kileleni katika msimamo wa ligi kuu, ninaamini ndiyo malengo yetu makubwa katika kuutetea ubingwa wetu.
“Hivyo, basi kikubwa nilichokipanga ni kuwa nitapambana kuhakikisha ninafunga bao au ninatengeneza nafasi ya bao kwa wachezaji wenzangu, kikubwa tunachokiangalia ni pointi tatu pekee.
“Timu yetu bila kuangalia nani kafunga, sisi tunaangalia ushindi utakaotuwezesha pointi tatu pekee, niwaondoe hofu Wanayanga wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutusapoti, ninaamini uwepo wao utafanikisha mengi,” alisema Ajibu.
Champion
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi