HAYA HAPA MAMBO MANNE YALIYOJIRI LEO KUTOKA TIMU YA YANGA
KAMBI YAO
Klabu ya Yanga jana ilifanya kikao na waandishi wa Habari makao makuu ya Klabu yao na kueleza kuwa kambi yao wameamua kuifanya mkoani Morogoro wakiamini ni sehemu sahihi kwao kuelekea mchezo dhidi ya Simba.
Awali Yanga waligoma kusema mahali hasa ilipo timu yao wakihofia kuhujumiwa na wapinzani wao Simba watakaopambana siku ya Jumamosi Oktoba 28. Mkwasa alizungumzia hiyo Ishu
KUREJEA KWA WACHEZAJI WALIOACHWA DAR
Wachezaji Donald Ngoma, Amis Tambwe na Thaban Kamusoko tayari wameungana na wenzao walioko mkoani Morogoro kwaajili ya Maandalizi ya mchezo wa watani wa JADI jumamosi, Dismas Ten amesema daktarai amethibitisha kuwa wachezaji wote wako fiti kuelekea mchezo kati ya Yanga na Simba Jumamosi.
Kamusoko,Ngoma na Tambwe waliachwa katika mechi za kanda ya ziwa kutokana na kuwa majeruhi, wachezaji hao walikosa mechi dhidi ya KAGERA SUGAR NA STAND UNITED.
WASHABIKI WATAKIWA KUNUNUA TIKETI MAPEMA
Mkwasa ambaye ndiye katibu mkuu wa Yanga amewataka wapenzi na washabiki wa Yanga kununua Tiketi mapema kwakuwa uwanja wa Uhuru hauchukui washabiki wengi huku akiwaomba ambao hawatapata tiketi kubakia Nyumbani ili kuepusha usumbufu.
TIMU YA WANAWAKE IKO MBIONI
Yanga pia inampango wa Kuja na timu ya wanawake itakayojulikana kama Yanga Princesses ambapo mchakato wa Kuipata timu hiyo tayari umetangazwa.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi