HABARI KUBWA YANGA NA TETESI ZA USAJILI LEO
TAARIFA KWA UFUPI KUHUSU KAMBI MOROGORO
Klabu Ya Yanga leo imeendelea kwa mazoezi huko Mjini Morogoro, Yanga Imefanya Mazoezi asubuhi ya Leo na Inatarajia kuendelea na mazoezi Jioni, Yani ni dozi ya mara mbili kwa Siku. Wanachama wa Yanga Mkoani Morogoro wameishukuru Klabu hiyo kwa kufanya maamuzi ya Kuipeleka Kambi ya Yanga Morogoro licha ya Kuwepo maeneo mengi Tu Tanzania.
TETESI ZA USAJILI YANGA 28.7.2017
Mchezaji wa Yanga Matheo Anthony ambaye mwanzoni ilisemekana ataachwa na Kikosi cha Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake, Kuna Taarifa za Ndani kuwa Yanga wameamua Kuendelea Naye kwaajili ya Msimu Ujao baada ya mchezaji Huyo Kusaini Miaka 2.
Yanga wanatarajiwa Kumalizia Kumtangaza mchezaji wa Mwisho kabisa kumsajili Jumapili Hii, Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili zimesema atakuwa ni mchezaji mzawa yani Mtanzania, Ila Tayari zimeshavuja kuwa Atakuwa ni Raphael Alpha Daudi toka Mbeya City ya Jijini Mbeya
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi