SHABIKI WA KRC GENK AMKUBALI SAMMATA
Jina la nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta limeendelea kuchukua headlines kutokana na kuonesha mchango katika timu hiyo.
Moja kati ya kitu ambacho kinatafsiriwa kuwa ni heshima na sifa kubwa kwa shabiki wa soka hususani barani Ulaya ni kupata jezi ya mchezaji anayempenda akiwa kaipata moja kwa moja kutoka kwa mchezaji husika iwe imesainiwa au katoka kuchezea mechi.
Samatta ameonekana kukubalika na mashabiki wa soka Ubelgiji kiasi cha shabiki kuingia na bango uwanjani akiwa kaandika “Samatta naweza kupata jezi yako tafadhari?”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi