MAMBO 5 YA KUMFANYA MWANAMKE AVUMILIE KWENYE NDOA
Mahusiano
mazuri kwa wanandoa au watu walio kwenye mahusiano ya kimapenzi ni moja
ya mambo yanayochangia wahusika pia kuwa na afya njema na hata kuepuka
baadhi ya matatizo kiafya.
Leo nmeona nikuletee mambo matano muhimu ambayo mwanamke hupenda atimiziwe na mume wake.
1. Kudekezwa & Kubembelezwa
Wanawake
hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, lakini pia wengi
hupenda kuungwa mkono katika maamuzi yao au mawazo yao. Hivyo basi ili
mwanaume uweze kumteka mwanamke wao ni lazima ujitahidi kuwa mkarimu na
mwenye lugha nzuri za kubembeleza kwa mkeo.
2. Kusikilizwa shida
Wanawake
hupenda pale wanapoeleza shida zao wasikilizwe vizuri na kutatuliwa
matatizo yao. Inawezekana hayo matatizo yakatatuliwa kwa kuwezeshwa
kifedha au hata ushari pia wakati mwingine.
3. Kuwa mstari wa mbele
Wanawake
muda wote hupenda kuoneshwa kuwa wao ni wathamani kuliko wengine hivyo
huhitaji kuwekwa mstari wa mbele katika mambo yao. Hali ambayo huwafanya
wao kuhisi wanapendwa zaidi.
4. Kufurahishwa kwenye ndoa
Hakikisha
wewe kama ni mwanaume basi katika sekta hii uwe umekamili kiasi cha
kutosha yaani hata kama huna fedha, lakini hakikisha eneo hili unaliweza
vizuri na unalifanya kwa ufanisi zaidi kila unapokutana na mkeo. Kwani
uwapo dhaifu eneo hili basi ni rahisi sana kuyumbisha mahusiano yenu au
ndoa yenu.
Kimsingi wewe kama mwanaume ni lazima utambue kuwa unawajibu wa kuhakikisha unamridhisha mpenzi/mke wako katika tendo hilo.
5. Nafasi ya kuzungumza
Kwa
kawaida wanawake hupenda zaidi kujieleza kuhusu hisia zao au mambo yao
kwa wale wanaohisi wanawapenda, hivyo mwanaume lazima uhakikishe
unatenga muda wa kuzungumza na mpenzi wako na kumsikiliza kuhusu mambo
yake na kuyafanyia kazi pale yanapoonekana yanawezekana.
Kimsingi
mambo hayo yote au machache kati ya hayo yakitokea yakakosekana ndani
ya ndoa kwa mda wa kipindi fulani huweza kupelekea mwanamke kuondoka na
ndoa kuvunjika hivyo ni muhimu kwa wanaume kuyazingatia hayo.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi