WAFANYAKAZI WANNE WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA
Wafanyakazi wanne wa Chama Cha Akiba na Mikopo cha Turiani, wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya wizi wa zaidi ya shilingi milioni 270 mali ya Wanachama wa Chama cha Akiba na mikopo cha Turiani (TUR-SACCOS).
Akisoma taarifa ya ukaguzi na uchunguzi wa wizi huo Afisa wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bwana Peter Nankunga amesema wafanyakazi hao walijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia akaunti bandia ambapo Neema Eyembe (karani wa fedha wa chama) alijipatia shilingi milioni 121.8, Nicholus Sifuni (Meneja wa chama) milioni 82.6 Erondy Elikana malikia,(mwenyekiti wa chama) milioni 51 na Paul Msuya (mhasibu wa chama) shilingi milioni 15.1.
Akiongea mara baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo ya ukaguzi na uchunguzi ambayo imesomwa kwenye Mkutano maalumu wa Wanachama wa Sacoss hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwalimu Mohamed Utali akaagiza wafanyakazi hao wakamatwe huku akisisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya kulinda na kuhakikisha vyama vya Ushirika vinakuwa mkombozi wa kiuchumi kwa wananchama wake.
Kwaupande wake Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bwana Donald Deogratia amesema wizi ni kosa kisheria na hivyo akashauri sheria ichukue mkondo wake dhidi ya watuhumiwa hao huku Kaimu Mwenyekiti wa TUR-SACCOS Bwana Octavian John akisema hatua ya kukamatwa kwa wafanyakazi hao itajenga imani ya wanachama juu usalama wa fedha zao.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi