MAMA AMWAGIA BINTI YAKE SUPU YA MOTO
Kulingana na ripoti, mwanamke mwenye umri wa makamo kwa jina Tricia Oterneghoro, alimmwagilia supu moto binti yake kwa kukosa kumtii na kulala katika nyumba ya jirani.
Kulingana na Joyce Emmanuel mwenye miaka 13, mama yake alikuwa amemmmwagilia supu kwa sababu alikuwa ameenda kulala kwa jirani alipomfungia nje kwa kusisitiza alikuwa akienda nje kuoga usiku.
Alisema:
“Ilikuwa wakati wa jioni na nikasema nataka kuoga lakini mama yangu akasema hapana. Nilienda nje kuoga lakini mama yangu akafunga mlango. Baada ya kubisha mara kadha, nilienda kulala katika nyumba ya rafimi yangu. Asubuhi mama yangu alikuja na kunimwagia supu moto mwilini,”
Kulingana na jirani mmoja aliyekimbia kumwokoa Joyce baada ya shambulizi la mama yake, alisema wamekuwa wakimwonya kila mara Tricia dhidi ya kumdhulumu binti yake.Walisema:
“Mwanamke mwenye akili timamu hawezi kumtendea hivi binti yake. Nimemwonya asimpige msichana huyo tena. Baba yake alipiga simu jana na msichana huyo akasema angependa kujiunga na chuo cha uuguzi.”
Akikiri kosa lake, Tricia alisema hakujua kilichomfanya kutenda hivyo, akiongeza kuwa alikuwa amewatahadharisha majirani zake hapo awali kutomrughusu Joyce kulala vyumbani mwao.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi