KAIMU MKUU WA IDARA YA ARDHI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUSEMA UONGO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry |
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry ameagiza kusimamishwa kazi kwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wilaya ya Sikonge kwa kosa la kutoa taarifa ya uongo kuhusu zoezi la upandaji miti wilayani humo.
Mwanry ametoa agizo hilo la kusimamisha kazi kaimu mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Fredy Masanja baada ya kumdanganya kuwa halmashauri hiyo ina Kitalu cha miti elfu kumi na mbili na miatisa [12,900] lakini cha kushangaza baada ya kufika eneo hilo hapakuwa na mche hata mmoja.
Ili kujiridhisha zaidi Mkuu wa mkoa akawataka viongozi wa wilaya ya Sikonge kumthibitishia kama wanakitambua kitalu hicho.
Kufuatia hali hiyo Mwanry akatoa agizo kwa katibu tawala wa mkoa.
Kampeni ya Upandaji miti ni Agizo la makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kila wilaya inapaswa kupanda miche Milioni 1.5.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi