GAZETI LA UINGEREZA LAANDIKA MAKALA KUHUSU MBWANA SAMATTA
Jarida maarufu nchini Uingereza la Daily Maillimemsifu mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Tanzania, Mbwana Samatta kwa mchango wake mkubwa aliouonyesha jana usiku kwa kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa 5-2.
Katika mchezo wa Europa League kati ya Genk na Gent zote za nchini Ubelgiji, Mbwanan Samatta alipachika kimiani magoli mawili na kuiwezesha timu yake ya Genk katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata, kwani katika mchezo wa marudiano ambao watakuwa nyumbani, watahitaji sare, suluhu au ushindi kuweza kusonga mbele.
Katika mchezo huo, Samatta ambaye amekuwa akifanya vizuri siku za hivi karibuni alipachika magoli mawili, moja likiwa ni kipindi cha kwanza dakika ya 41 na jingine dakika ya 72 kipindi cha pili.
Timu hizi zitacheza mchezo wa marudiano Machi 16 mwaka huu wakati ambao Gent itasafiri kuwafuata Genk katika uwanja wao wa nyumbani ili kukamilisha mzunguko wa pili
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi