BREAKING NEWS:AJALI YA BASI NA LORI MISUNGWI

Basi la ALLY'S STAR GULF AIR lenye namba za usajiri 514 ANW lifanyalo safari zake kati ya Mwanza na Tabora, limepata ajali asubuhi ya leo saa moja katika kijiji cha MWAZENZE wilayani Misungwi Mwanza mara baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mizigo na kuacha njia.

Kwa mujibu wa maelezo ya abiria waliokuwa wamepanda kwenye basi hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva alipokuwa akijaribu kuovateki gari iliyokuwa mbele yake pasipokujua mbele yake zaidi kuna nini, ndipo basi hilo likakutana ghafla na lori la AZAM lililokuwa limebeba unga wa ngano.

Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyefariki wala kuumia zaidi ya mtu mmoja kupata mshituko wa mguu. Dereva alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo kutokea.

Mwandishi wetu wa MASENGWA BLOG Isaac Luhende, alifika eneo la tukio robo saa baada ya ajali hiyo kutokea ametuletea picha kadhaa za tukio hilo.

Lori la mizigo lililogongana na basi hilo likiwa limeharibika baada ya ajali


Basi likiwa limeacha njia baada ya ajali

Watu wakistaajabu maajabu ya Mungu kwa jinsi basi lilivyoharibika lakini hakuna mtu aliyeumia


Huu ndio uso wa basi, ukiwa umeharibika


Tingo wa basi hilo akiwa anapakua mizigo kutoka kwenye buti ya basi

Basi likiwa nje ya barabara, baada ya kupata ajali na kuacha njia
Sehemu kubwa ya basi iliyoharibika mara baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mizigo

Hivi ndivyo basi lilivyoharibika




Lori la mizigo na jinsi lilivyoharibika

Lori la AZAM lililokuwa limebeba unga wa nano likielekea Kwanzaa mara baada ya ajali


PICHA ZOTE NA ISAAC LUHENDE
MASENGWA BLOG.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.