WANNE KIZIMBANI KWA KUMKASHIFU RAISI


Dar es Salaam. Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU) kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shitaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo(19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel(21) na Anne Mwansasu(21), ambapo wamepandishwa mahakamani hapo leo  na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja.

Kwa pamoja washtakiwa hao  wanadaiwa kuchapisha picha ambazo zinaonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa hijabu kama mwanamke wa Kiislamu na kuzisambaza kwenye mtandao huo wa WhatsApp,  huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kitimiza masharti ya dhamana.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.