MARTINE KADINDA AFUNGUKA KINACHOMPONZA WEMA SEPETU
MWANAMITINDO Martin Kadinda, amefunguka kuwa kinachomponza Wema hadi ajikute anaingia kwenye misala mbalimbali ya kipolisi ni watu wanaomzunguka.
Kadinda ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, alisema ili Wema aweze kufanikiwa maishani, hana budi kuwaweka pembeni baadhi ya marafi ki ambao wana tabia chafu kwani mara nyingi wamekuwa wakimsababishia matatizo mbele ya jamii.
“Siwezi kuwataja majini lakini Wema mwenyewe naamini anawajua marafi ki zake ambao si wazuri, wanaomwingiza kwenye majanga mara kwa mara, ni vyema akaachana nao ili ‘kumaintain’ heshima ya jina lake,” alisema Kadinda.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi