MWENYEKITI WA CCM MKOA WA KIGOMA AFARIKI DUNIA


Kigoma. Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Samson Naingo (76) amefariki dunia akiwa anapata matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kigoma, Maweni.

Akitoa taarifa ya kifo chake, msemaji wa familia, Amon Ndinande amesema merehemu alikuwa anasumbuliwa na kisukari na shinikizo la damu, hali iliyosababisha kupata ugonjwa wa kiharusi.

Amesema kabla ya kufikwa na mauti marehemu alilazwa hospitali ya Maweni alipokuwa akipatiwa matibabu, kuanzia Februari 10 mwaka huu hadi alipofariki dunia.

Naingo aliitumikia CCM kwa miaka 20 akiwa kiongozi wa wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.