HII KALI YA MWAKA!! MZEE WA MIAKA 98 AFUNGA NDOA NA BIBI WA MIAKA 88


Mzee Willy Kinyua (98) amefunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.

Wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya.

Wanandoa hao wenye watoto watano wanatembea kwa kutumia fimbo.

Kinyua amesema, alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura hakumsaliti.

“Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti ” amesema mzee huyo baada ya kufunga ndoa.

“Nampenda (Nyambura) kwa sababu ni mrembo sana. Nimfunue sura yake umuone” alimuuliza muongoza ibada akijibu swali la kiongozi huyo wa kiroho.

Nyambura amesema, amefurahi kusheherekea ndoa yake kama ambavyo kila mwanamke angependa iwe hivyo.

Bibi hiyo amesema, alimpenda sana Kinyua na kwamba wamekuwa wakiishi kwa amani.

Kwa mujibu wa Nyambura, ndoa zinavunjika kwa sababu wanaume wengi wanawasaliti wake zao kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine.


IMEANDIKWA NA BASIL MSONGO wa gazeti la habarileo

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.