Mhubiri mmoja wa
zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye alikuwa na takriban wanawake
86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.
Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake.
