Ofisi ya rais wa
zamani wa Marekani Barack Obama imetoa tamko na kusema kwamba raisi
huyo wa zamani anakerwa na na maandamano yanayoendelea nchini humo
kupinga tamko la raisi Donald Trump kutaka kuweka vizuizi vya uhamiaji
juu ya wasafiri kutoka kwa baadhi nchi za Kiislamu.
Msemaji wa
raisi Barack Obama, Kevin Lewis, amesema kwamba raisi mstaafu Kimsingi
hakukubaliana na wazo la ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya dini yao.
Na kuongeza kusema kwamba wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya
kusikilizwa na viongozi waliochaguliwa na ndiyo matarajio yao pindi
waonapo Marekani inaingia hatarini hatarini.