Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amesema tukio la mwanafunzi huyo kuuawa lilitokea jana katika kijiji cha Karutanga wilayani Buleba na kumtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Remijius Poncian(16).
Kamanda Olomi amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni baba wa kambo, Hassan Misigaro (52) anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
