OMBEN SEFUE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA CHUO CHA DIPLOMASIA


Image result for sefue ombeni
Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli amemteua aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kuwa mwenyekiti nwa bodi ya chuo cha diplomasia

Balozi Sefue amepata uteuzi huo jana ikiwa ni miezi kumi tangu Rais Magufuli atengue uteuzi wake [kama Katibu Mkuu Kiongozi]kwa sababu ambazo hazikutajwa huku akiahidi kumpangia kazi nyingine na nafasi yake ikajazwa na Balozi John Kijazi, . 


Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo, Balozi Augustine Mahiga amewateua wajumbe sita wa Bodi ya chuo hicho cha Diplomasia. 


Wajumbe hao ni Balozi Begum Taj, Balozi John Haule, Juma Salum, Profesa Mohamed Bakari, Profesa Innocent Zilihona na Mathias Abias. 


Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Oktoba 6 mwaka huu. 

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.