KICHUYA AISHI KAMA MFALME
Mshambuliaji wa timu ya SIMBA SPORTS CLUB ''Kichuya'' amegundua kubadilika maisha yake baada ya kurejea
kwao Morogoro, mara tu baada ya mechi ya Yanga dhidi ya Simba ambayo
yeye alifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho na matokeo kuwa
1-1.
Kichuya kama kama mfalme, kwani hats madereva taxi na wale wa bodaboda hawataki malipo wanapomchukua.
Inaonekana watu wa Morogoro hata wasio mashabiki wa Simba wanajivunia kutokana na kazi nzuri anayoifanya.
Kichuya amekuwa na mafanikio makubwa katika mechi chache tu alizoichezea Simba kutokana na mchango wake mkubwa katika upachikaji mabao pamoja na kutoa pasi.
Hata hivyo, Kichuya amekuwa akisema kwamba hawezi kubweteka hata kidogo kutokana na namna watu wanayoonyesha kumjali badala yake ataongeza juhudi zaidi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi