ASKARI 9 WA JESHI LA POLISI WANUSURIKA KIFO AJALI YA GARI KWENYE MBIO ZA MWENGE WA UHURU SHINYANGA
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
AJALI YA GARI LA POLISI KUACHA NJIA / KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI.
TAREHE 05/10/2016 MAJIRA YA 09:50 KATIKA KIJIJI CHA SHILABELA, KATA YA PANDAKICHIZA, TARAFA YA NINDO, WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI MKOA WA SHINYANGA GARI NAMBA PT. 1886 TOYOTA LAND CRUISER MALI YA MKUU WA POLISI WILAYA YA SHINYANGA LIKIENDESHWA NA DEREVA WA POLISI LIKIWA KWENYE SHUGHULI ZA MWENGE WA UHURU LILIACHA NJIA NA KUGONGA GEMA UPANDE WA KULIA MWA BARABARA , KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA ASKARI:
(1)PF. 18763 INSP ZITTA AMBAYE AMEUMIA MKONO WA KULIA
(2)WP.10550 PC MARIAM AMBAYE AMEUMIA KIUNO
(3)H.6012 D/C YENYE AMBAYE AMEUMIA KIFUA NA GOTI LA MGUU WA KULIA
(4)G.1660 PC PAULO AMBAYE AMEUMIA KICHWANI
(5)G.7091 PC JOHN AMEUMIA GOTI MGUU MGUU WA KUSHOTO NA MCHUBUKO KATIKA VIDOLE VYA MKONO WA KULIA
(6)H.4740 PC FREDY - AMEUMIA BEGA LA KULIA NA MICHUBUKO MKONO WA KUSHOTO (7)G.4381 PC MOHAMED - AMEUMIA MAKALIO MGUU WA KULIA
(8)H.5937 D/C JOSEPHAT - AMEUMIA GOTI LA MGUU WA KULIA NA
(9)J.1101 PC ALBANO - AMEUMIA BEGA LA KUSHOTO .
HALI ZA MAJERUHI ZINAENDELEA VIZURI AMBAPO WAMEPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA NA KURUHUSIWA KWANI HALIZAO NI NZURI KASORO ASKARI WATATU AMBAO BADO WANAFANYIWA UCHUNGUZI ZAIDI LAKINI HALI ZAO SI MBAYA.
KIINI CHA AJALI HIYO NI BARABARA AMBAYO SI NZURI.
UHARIBIFU WA GARI PIA SI MKUBWA.
IMETOLEWA NA MULIRO J MULIRO (ACP) RPC SHINYANGA.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi