MWANAFUNZI ASIMULIA JINSI ALIVYOPIGWA, MKUU WA SHULE HIYO AVULIWA MADARAKA



Serikali ya Tanzania imeagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kanda ya video ilioonyesha kundi moja la walimu likimpiga mwanafunzi.



Mwalimu mkuu wa shule hiyo tayari amesimamishwa kazi kwa mda kwa kutochukua hatua hata baada ya kugundua kuhusu kisa hicho ,taarifa ya serikali imesema.

Raia wa Tanzania katika mitandao ya kijamii walionyesha hasira zao ,wakiitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya washambuliaji hao.

Video hiyo ambayo haijakaguliwa inaonyesha mwanafunzi mmoja akipigwa na kundi la walimu katika kile kinachoonekana kuwa chumba cha wafanya kazi wa shule.

Katika kanda hiyo ya sekunde 38,takriban watu watano wanaonekana wakikabiliana na kushambulia mvulana huyo aliyeanguka chini kwa kumpiga ngumi pamoja na mateke.

Adhabu ya kupigwa viboko ni haramu nchini Tanzania,na kisa hicho cha hivi karibuni kinatarajiwa kuzua mjadala kuhusu utekelezwaji wa sheria hiyo katika shule za taifa hilo.


ANGALIA HAPA VIDEO YA MWANAFUNZI ALIYEPEWA KIPIGO NA WALIMU AKISIMULIA MKASA HUO

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.