
Watoto wawili wa familia moja wa kitongoji Ihula kijiji cha Bulumbaka kata Mwaubingi halmshauri ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wamefariki kwa kudumbukia kwenye shimo la maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali za kuchenjua dhahabu kwenye mgodi wa Gasuma no moja uliopo kwenye halmashauri hiyo.
Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu ASF Faustin Mtitu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akitaja chanzo kuwa ni kunywa maji hayo na kukosa hewa ya oksijeni.
Watoto ni wa familia moja ambao ni hao ni Yona Chai (7) na Baraka Balida (3).
0 Comments