MZIZE ANA OFA TATU UTURUKI, ZIFAHAMU HAPA


INEALEZWA kuwa mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize anatajwa kuhitajika na Klabu Tatu kubwa kutoka Ligi Kuu ya Uturuki na tayari ofa zimeanza kuinga katika timu hiyo.

Kwa mujibu wa Chanzo cha Habari kutoka ndani Kamati ya Utendaji ya Yanga, Klabu za Fenerhbahce, Galatasaray na Besiktas ni kati ya zinatajwa kuwania saini ya mshambuliaji huyo.

Mzize ni kati ya washambuliaji waliokuwepo katika vita ya kuwania Ufungaji Bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu ambaye amefunga mabao 10 sawa na Prince Dube huku Charles Ahoua akiongoza akipachika 12.

Post a Comment

0 Comments