Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt Emmanuel Makala amewataka Wachungaji wote wa Dayosisi yake kuwafundisha wakristo neno la MUNGU kwa usahihi bila kupindisha ukweli ili Wakristo waweze kuuona ukuu na uweza wa MUNGU katika maisha yao.
Askofu Dkt Makala ameyasema hayo katika Ibada ya ubarikio wa Mchungaji mpya Innocent Kimaro iliyofanyika Jumapili tar 23/10/2022 KKKT Usharika wa Maganzo Shinyanga ambapo Katika Ibada hiyo Askofu Dkt Makala amempongeza Mch Innocent kwa hatua hiyo na pia kumtaka kutumika kikamilifu mbele za MUNGU na kulinda Ushuhuda siku za maisha yake.
Ibada hiyo imehudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, wajumbe wa Halmashauri kuu ya Dayosisi, Watheolojia pamoja na Wakristo ambapo pia kwa pamoja wamempongeza na kumtakia Baraka Katika utumishi alioitiwa na MUNGU.
Msaidizi wa Askofu Dkt Yohana Ernest Nzelu (kushoto), Msaidizi wa Askofu mstaafu Mchungaji Trafaina Assery Nkya (katikati) na Mchungaji wa usharika wa Maganzo
Katibu mkuu wa Dayosisi Bi Happiness Geffi akisoma wajibu wa Kwa Mchungaji aliyeibarikiwa Innocent Kimaro
Innocent Kimaro wakati wa ubarikio wake wa kuwa Mchungaji
Wachungaji wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakimwombea Mchungaji aliyeibarikiwa Innocent Kimaro
Mchungaji aliyeibarikiwa Innocent Kimaro akisaini kiapo cha uchungaji
Tags:
habari